• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajibu hatua za Marekani za kuziwekea vizuizi ofisi za vyombo vya habari vya China nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-03-18 09:10:39

    China imetangaza kuchukua hatua kujibu vitendo vya Marekani vya kuziwekea vizuizi ofisi za vyombo vya habari nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na China inasema katika miaka ya karibuni serikali ya Marekani imeweka vizuizi visivyo vya ulazima dhidi ya ofisi za vyombo vya habari vya China na wanahabari wa China nchini Marekani, kuwaongeza ugumu wa kazi kwa makusudi wanahabari wa China, na kuzidisha ubaguzi na ukandamizajii wa kisiasa dhidi yao.

    Taarifa imesema kutokana na sababu hizo, China inachukua hatua zifuatazo ambazo zinafanya kazi mara moja.

    Kwanza, China inayataka matawi ya VOA, New York Times, the Wall Street Journal, the Washington Post and Time kutoa taarifa za maandishi kwa idara husika ya China kuhusu wafanyakazi wao, fedha, kazi na mali zao nchini China.

    Pili, China inawataka wanahabari wenye uraia wa Marekani wanaofanya kazi kwenye ofisi za the New York Times, the Wall Street Journal and the Washington Post ambao muda wa hati zao za uandishi wa habari utaisha mwishoni mwa mwaka 2020 kuripoti kwa Idara ya Habari ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China ndani ya siku nne kuanzia leo Jumatano na kurudisha vitambulisho vyao vya uandishi wa habari ndani ya siku kumi. Watu hao hawataruhusiwa kuendelea na kazi kama wanahabari nchini China, ikiwemo HongKong na Macao.

    Tatu, ili kujibu vizuizi vya kibaguzi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya wanahabari wa China kwenye masuala ya visa, mapitio ya kiutawala na kutoa ripoti, China itachukua hatua sawa na hizo dhidi ya wanahabari wa Marekani.

    Taarifa inasema hatua hizo za China ni halali na za kujilinda, na zinalenga kujibu hatua za ubaguzi na ukandamizaji zinazochukuliwa na Marekani dhidi ya vyombo vya habari vya China nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako