• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo vya COVID-19 nchini Iran yakaribia 1,000

    (GMT+08:00) 2020-03-18 09:27:03

    Iran jana iliripoti watu 1,178 zaidi waliothibitishwa kuambukizwa COVID-19 na vifo vya watu 135 kutokana na virusi hivyo, na kuifanya idadi ya jumla ya vifo kutokana na COVID-19 nchini humo ikaribie 1,000.

    Wizara ya afya na elimu ya matibabu ya Iran imetangaza kuwa maambukizi ya COVID-19 yameongezeka na kufikia 16,169, na idadi ya vifo imefikia 988.

    Qatar jana imeripoti watu watatu waliothibitishwa kuambukizwa COVID-19, na idadi ya jumla ya maambukizi nchini humo imefikia 442.

    Uturuki imeripoti kifo cha kwanza na maambukizi 51 zaidi ya COVID-19, na idadi ya maambukizi nchini humo imefikia 98. Israel pia imesema idadi ya maambukizi ya COVID-19 nchini humo imefikia 337.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako