• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaripoti maendeleo mapya katika dawa na tiba ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-18 09:37:23

    China imemaliza utafiti wa kimatibabu wa dawa ya virusi ya Favipiravir, ambao imeonesha ufanisi dhidi ya nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vya korona.

    Mkurugenzi wa Kituo cha taifa cha Maendeleo ya Baioteknolojia chini ya Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya China Bw. Zhang Xinmin amesema, Favipiravir, ambayo ni dawa ya kutibu mafua iliyoidhinishwa mwaka 2014, imeonesha kuwa haina athari kwa watumiaji kwenye majaribio ya kimatibabu yaliyoshirikisha wagonjwa zaidi ya 80 mjini Shenzhen.

    Bw. Zhang amesema dawa ya Favipiravir imependekezwa kutumiwa kwenye matibabu ya COVID-19, na inatarajiwa kuwekwa kwenye mpango wa utambuzi na tiba ya ugonjwa huo haraka iwezekanavyo. Ameongeza kuwa kampuni moja ya dawa imeidhinishwa na Mamlaka ya Bidhaa za Kimatibabu China kutengeneza dawa hiyo na kuhakikisha ugavi wake sokoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako