• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: FKF yamuomba rais Uhuru awalipie deni

    (GMT+08:00) 2020-03-18 16:19:20

    Shirikisho la Soka Kenya (FKF) sasa limemgeukia rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta kuhusu malipo ya Sh za Kenya milioni 109 wanazodaiwa na kocha wa zamani wa Harambee Stars, Adel Amrouche baada ya kumfukuza bila ya kufuata taratibu. Rais wa Shirikisho hilo, Nick Mwendwa amemuomba rais Kenyatta kuwalipia deni hilo ili kuinusuru Kenya isifungiwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA). Kushindwa kumlipa kocha huyo kabla ya siku ya mwisho iliyowekwa ambayo ilikuwa Machi 11 kunaweza kuifanya Kenya kufungiwa kushiriki mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako