• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yahimizwa kuchukua hatua mapema kukabiliana na COVID-19 huku ikiendelea kupambana na malaria

    (GMT+08:00) 2020-03-18 18:06:34

    Wanasayansi 14 kutoka China, Singapore, Ujerumani, Gabon, Senegal na Uingereza wametoa makala kwenye jarida la tiba la The Lancet, kuzitahadharisha nchi za Afrika kuchukua hatua mapema kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 na kuendelea kutia nguvu katika mapambano dhidi ya malaria.

    Mtaalam wa taasisi ya Artemisinin ya China Bibi Tu Youyou amesema, kutokana na maambukizi ya haraka ya ya COVID-19 duniani, Afrika inapaswa kujiandaa mapema. Pia ugonjwa huo unaweza kuathiri jitihada za kudhibiti malaria, hivyo ni bora kwa nchi za Afrika kuchukua hatua nyingine kukabiliana na changamoto hiyo.

    Pia amesema, dalili kuu za kuambukizwa COVID-19 ni homa, maumivu ya misuli na uchovu ambazo zinafanana na ugonjwa wa malaria, jambo linaloongeza ugumu wa utambuzi wa virusi hivyo. Licha ya hayo, nchi za Afrika zinapaswa kuhimiza watu kuongeza umbali wakati wa mazungumzo, kuvaa mask na kwenda hospitali mapema pindi wanapojisikia vibaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako