• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa larekebisha kazi ili kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-18 18:09:22

    Ujumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa ambayo ni nchi ya mwenyekiti ya zamu wa Baraza la Usalama la Umoja huo kwa mwezi huu umesema, Baraza hilo linarekebisha utaratibu wa kazi ili kukabiliana na maambukizi ya COVID-19, na pia linaendelea kutekeleza majukumu yake.

    Ujumbe huo umesema, China, ikiwa nchi mwenyekiti wa Baraza la Usalama inajua majukumu ya Baraza hilo na inafanya majadiliano na nchi nyingine wajumbe kuhusu utaratibu wa kazi za Baraza hilo. Kutokana na maambukizi ya virusi vipya vya korona na mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama linapaswa kuchukua hatua za lazima ili kuzuia kuenea kwa maambukizi hayo.

    Aidha nchi wajumbe wa Baraza hilo pia zilifanya majadiliano kuhusu miswada ya maazimio kuhusu suala la Somalia na suala la Darfur na kuamua kuchukua hatua wiki ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako