• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bado wanawake ni wachache sekta ya ujenzi Kenya

    (GMT+08:00) 2020-03-18 19:02:50

    Utafiti mpya nchini Kenya umeonesha kuwa wanawake walio kwenye sekta ya ujenzi ni wachache.

    Utafiti huo uliotolewa na chama cha wanawake walio katika sekta hiyo unaonyesha kuwa licha ukuaji wa sekta hiyo ambayo imekuwa na ukuaji mkubwa ndani ya miaka kadhaa iliyopita bado haina wanawake wengi.

    Makamu wa rais wa chama hicho Bibi Emma Miloyo amesema utafiti huo umewasaidia kupata habari kuhusu kiwango cha wanawake kwenye Nyanja mbalimbali katika sektaya ujenzi.

    Taakwimu kutoka kwa halmashauri ya wahadisi nchini Kenya zinaonesha kuwa kuna asilimia 10.6 tu ya wanawake wanaohitimu na shahadda za uhadisi ambayo ni sawa na 1,500 tu kati ya wanafunzi 14,320 .

    Na kati ya kandarasi 17,100 za ujenzi zilizosajiliwa na mamlaka ya ujenzi ya kitaifa mwaka 2019 ni 2,600 tu za wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako