• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wachuuzi Dodoma waonywa

    (GMT+08:00) 2020-03-18 19:04:11
    Halmashauri ya Jiji la Dodoma, limetoa onyo kwa wafanyabiashara wadogo (Machinga) kuacha kupanga bidhaa zao kabla ya muda uliopangwa kwenye barabara ya Nyerere Square ili kutozuia watumiaji wengine wa barabara.

    Katika barabara hiyo, wafanyabiashara hao wanapaswa kupanga bidhaa zao kuanzia saa 10:00 jioni baada ya muda wa kazi kuisha, lakini wameonekana kukiuka utaratibu huo na kuanza kupanga kabla ya muda huo.

    Onyo hilo lilitolewa jana na Ofisa Masoko wa Jiji la Dodoma, James Yuna, alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara hao wanaofanya biashara katika eneo hilo.

    Alisema hivi sasa wamekuwa wakipanga bidhaa muda wa asubuhi hali inayoleta usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako