• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashiriki kwenye ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na COVID-19 kwa hatua madhubuti

    (GMT+08:00) 2020-03-18 19:54:47

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, kitendo cha China kutoa misaada kwa nchi nyingine na mashirika ya kimataifa kadiri iwezavyo ni cha kujiwajibika, na pia kinasaidia kuimarisha mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya virusi vya korona (COVID-19), na China itaendelea kuongeza ushirikiano na pande mbalimbali.

    Geng amesema, hivi sasa virusi hivyo vinaenea kwa kasi katika nchi nyingi, na hadi sasa China imetoa misaada kwa nchi mbalimbali ikiwemo Pakistan, Laos, Thailand, Iran, Umoja wa Afrika na Shirika la Afya Duniani, na pia imeahidi kutoa misaada kwa nchi nyingine.

    Aidha, China imetuma vikundi vya madaktari kwa nchi zinazoathiriwa zaidi na ugonjwa huo, na kufanya mikutano kwa njia ya video na nchi nyingine, ili kutoa uzeofu wa kukabiliana na ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako