• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Li Keqiang afanya mazungumzo na mkuu wa tume ya Ulaya kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2020-03-19 08:48:25

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amefanya mazungumzo kwa njia ya simu ya mwenyekiti wa Tume ya Ulaya Bibi Ursula von der Leyen.

    Bw. Li Keqiang amesema juhudi za kudhibiti milipuko ya magonjwa hazina mipaka. Amesema katika hali ya sasa, China iko pamoja na Ulaya, na inaunga mkono juhudi za Ulaya kupambana na virusi vya korona. Amesema China itatoa urahisi kwa Ulaya kwenye manunuzi ya vifaa vya matibabu, na pia inapenda kufanya ushirikiano wa kimataifa ili kulinda kwa pamoja afya ya binadamu. Ameitaka Ulaya itilie maanani na kuhakikisha usalama na mahitaji ya maisha ya raia wa China walioko katika nchi za Umoja wa Ulaya.

    Kwa upande wake Bibi Ursula von der Leyen ameishukuru China kwa uungaji mkono wake kwenye mapambano dhidi ya virusi vya korona. Hivi sasa Ulaya bado inahitaji kununua vifaa vya matibabu, na inaitaka China kuendelea kutoa uratibu na msaada. Amesema kushikana mikono kati ya Ulaya na China kwenye mapambano haya, kumeonesha urafiki na ushirikiano mzuri kati ya pande hizo mbili.

      

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako