• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KORONA: Mchezaji wa Meizhou Hakka ya China agunduliwa kuambukizwa virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-03-19 08:57:51

    Matarajio ya msimu wa soka wa China kuanza mapema mwezi Aprili yameanza kufifia baada ya jana mchezaji kutoka Brazil kugundulika kuwa na virusi vya korona. Mchezaji huyo ambaye hakutajwa jina lake ambaye ana miaka 30 na kuishi mji wa kusini wa Meizhou yupo hospitali karibu na Guangzhou. Mshambuliaji huyo wa Meizhou Hakka ni mchezaji wa kwanza kuripotiwa na virusi hivyo katika ligi ya China. Meizhou Hakka ipo kwenye League One ya China. Mshambuliaji huyo alifika uwanja wa ndege wa Guangzhou akitokea Bangkok juzi Jumatatu na kupelekwa hospitali. Hivi sasa kikosi kizima cha Meizhou kipo karantini na msimu mpya unaweza kuchelewa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako