• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Huawei ya China yaisaidia serikali ya Kenya kufanya mkutano kwa njia ya video juu ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-19 09:52:18

    Maofisa wa afya wa China na wataalamu kutoka nchi zaidi ya 20 za Afrika jana wamefanya mkutano kwa njia ya video kuhusu COVID-19, ambao ulishirikiwa na ujumbe wa Kenya kwa kutumia vifaa vinavyotolewa na kampuni ya Huwei ya China.

    Waziri wa afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe na wataalamu wanaoshiriki kwenye mapambano dhidi ya virusi hivyo walihudhuria mkutano huo. Kwenye mkutano huo maofisa na wataalamu wa China wameeleza matokeo mapya na hatua za aina mbalimbali katika kudhibiti COVID-19. Bw. Kagwe amesema mkutano huo umewapatia watu ujuzi unaoweza kuwasaidia wananchi wa Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako