• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Madrid kumtoa bure Bale ili imsajili Mbappe au Salah

    (GMT+08:00) 2020-03-19 16:15:48

    Real Madrid iko tayari kumtoa bure Gareth Bale wakati wa usajili wa majira ya kiangazi ili kufungua milango ya usajili wa mshambuliaji wa timu ya Paris Saint German Kylian Mbappe au Mohamed Salah wa Liverpool. Kocha wa Real, Zinedine Zidane amesema timu hiyo iko tayari kumwondoa Bale bure wakati wa usajili wa majira ya kiangazi ili kutoa nafasi kwa usajili mpya. Uamuzi huo wa Madrid unasemekana kuwa habari njema kwa timu za Machester United na Tottenham ambazo zinatajwa kuwania saini za winga huyo wa kimataifa kwa kipindi kirefu. Bale alijiunga na Real Madrid mwaka 2013 kwa dau la pound milioni 85.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako