Msemaji wa jeshi la serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa Bw. Mohamed Gonono amesema jeshi hilo lilizuia shambulizi lililofanywa kusini mwa Tripoli na waasi wanaotokea sehemu ya mashariki ya nchi hiyo.
Katika taarifa yake, Bw. Gonono amesema jeshi hilo liliwazuia wapiganaji wa kundi la waasi linaloongozwa na kamanda Jenerali Khalifa Haftar katika mji wa mashariki wa nchi hiyo, waliovunja azimio la kusitisha vita na kufanya mashambulizi kwa kutumia makombora huko Ain Zara, kusini mwa Tripoli.
Kamanda wa jeshi la serikali Ahmad Abu-Shahma aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi hilo limedhibiti tena eneo la Ain Zara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |