• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wasio waadilifu watachukuliwa hatua kali za kisheria,asema Rais Kenyatta

    (GMT+08:00) 2020-03-19 19:14:43
    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameonya kuwa wafanyabiashara wenye tamaA na wakiritimba wanaohodhi bidhaa wakati huu Kenya na dunia nzima zikipambana na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 watachukuliwa hatua za kisheria.

    Kwenye kikao na wadu wa fedha jana,Rais Kenyatta alisema ni ukosefu wa utu nan i kinyume cha sheria kwa mfanyabiahsara yeyote kuongeza bei za bidhaa wakati nchi inapitia kipindi kigumu kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona,Covid-19.

    Rais ametoa kauli hiyo kutokana na kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameongeza maradufu bei za bidhaa kama vile sabuni za kuosha mikono na dawa za kuua viini.

    Wakati huo huo Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Dkt Patrick Njoroge,alisema kama hatua ya kudhibiti ueneaji wa Covid-19,taifa linapendekeza utaratibu wa kununua bidhaa na kulipia huduma kwa njia ya simu ambapo ada ya malipo yasiyozidi 1,000 imeondolewa kwa muda.

    Aidha Dkt Njoroge alitangaza kuwa ili kuimarisha uchumi pesa zitakazopelekwa benki kuanzia sasa zitahifadhiwa kwa muda wa wiki moja kabla ya kusambazwa.

    Pia alitoa maelekezo kwa benki na mashirika ya kifedha kuwapa muda wa mwaka mmoja wateja wao waliochukua mikopo kuanzia Machi 2,2020 ,ili waweze kulipa mikopo hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako