• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • COMESA kuwapiga faini ya hadi $300,000 wafanyabishara wanaouza bidhaa feki

    (GMT+08:00) 2020-03-19 19:15:05
    Kamisheni ya Ushindani ya Jumuiya ya nchi za Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) imetoa onyo kwa makampuni na watu binafsi ambao wanauza bidhaa ambazo hajizapimwa na kuthibitishwa,wanazodai zinaweza kutibu na kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.

    Kamisheni hiyo iliundwa na Jumuiya ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) ili kukuza na kuhimiza ushindani wa haki kwa kuondoa vizuizi vya biashara vinavyozuia ufanisi wa shughuli za masoko.

    Kamisheni hiyo inalenga kuongeza ustawi wa watumiaji katika soko la pamoja na kuwalinda watumiaji dhidi ya mwenendo mbaya wa watendaji wa soko.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa kamisheni hiyo,George Lipimle,alisema katika taarifa ,kuwa makampuni na watu binafsi wanafaa kujiepusha na kuuza bidhaa ambazo hazijathibitishwa.Alisema kamisheni hiyo haitasita kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na vikwazo na faini za hadi $300,000.

    Alitoa wito kwa watumizi katika soko hilo la pamoja kuwa makini na kuripoti visa vyovyote kwa kamisheni hiyo au kwa shirika lolote linalowalinda watumizi katika nchi wanazoishi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako