• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Waziri Mkkuu Kassim Majaliwa atoa wito kwa SADC kuungana kutokomeza Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-19 19:15:23
    Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, amezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuungana katika mapambano ya kuutokomeza ugonjwa wa virusi vya corona pamoja na kufuata masharti yatolewayo na wataalamu wa afya, vinginevyo utaathiri uchumi wa nchi.

    Alitoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC, uliokuwa unafanyika kwa njia ya video ukiwajumuisha Mawaziri wa Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

    Aidha, alisema katika miaka 40 tangu kuanzishwa kwa SADC mafanikio mbalimbali yamepatikana kama miradi mbalimbali ya miundombinu imeendelea kutekelezwa na kuiwekea kipaumbele sekta ya viwanda ambayo ni nguzo ya msingi katika kusaidia kukua kwa uchumi wa kanda na wa kila mwanachama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako