• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OLIMPIKI: Ugiriki yakabidhi mwenge wa olimpiki kwa waandaaji wa Olimpiki ya Tokyo

    (GMT+08:00) 2020-03-20 08:25:42

    Ugiriki jana Alhamis ilikabidhi mwenye wa Olimpiki kwa waandaaji wa Olimpiki ya Tokyo 2020 kwenye sherehe iliyofanywa bila watazamaji kufuatia wito wa wadau mbalimbali kutaka kuahirishwa kwa michezo hiyo kutokana na mlipuko wa virusi vya korona. Binga wa mchezo wa sarakasi wa Olimpiki Lefteris Petrounias alikimbia mzunguko mmoja bila ya kuwepo watazamaji na bingwa wa kuruka kwa upondo wa Olimpiki Katerina Stefanidi akawasha mwenge (lit a cauldron) ndani ya uwanja wa Panathenaic ambako michezo ya kwanza ya Olimpiki ilifanyika mwaka1896. Baadaye mwenge ukakabidhiwa kwa wawakilishi Naoko Imoto, ambaye ni mwogeleaji aliyeshindana kwenye Olimpiki ya Atlanta mwaka 1996. Kwenye taarifa yake rais wa Ugiriki Katerina Sakellaropoulou amesema thamani ya Olimpiki ya "concord, goodwill, brotherhood ndio silaha ya kutumia kupambana na virusi vya korona. Sherehe za kuwasha mwenge za wiki iliyopita katika Olympia ya kale pia zilifanywa bila ya watazamaji, huku Ugiriki ikiripoti kifo cha kwanza kutokana na virusi. Hata hivyo Mkuu wa Riadha Duniani Sebastian Coe amekiri jana kuwa Michezo ya Olimpiki inaweza kusogezwa mbele mwaka huu, lakini amesema ni mapema kutoa mamuzi ya uhakika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako