• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KORONA: Sion yasamehe wachezaji 9 kwa kukataa kukatwa mshahara, Ibrahimovic azindua kampeni ya kupambana na korona

    (GMT+08:00) 2020-03-20 08:27:01

    Klabu ya Sion ya Uswiss imewaacha wachezaji wake 9 waliokataa kukatwa mshahara wakati huu Ligi yao ikiwa imesimama kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya korona. Mastaa wa zamani wa Arsenal Alex Song na Johan Djourou ni miongoni mwa wachezaji wa klabu hiyo walioachwa kwa sababu ya kugoma kukatwa mishahara yao. Kwa mujibu wa SDA News na RSI TV Sion wamewaacha nahodha Xavier Kouassi, Pajtim Kasami, Ermir Lenjani, Seydou Doumbia, Mickael Facchinetti, Christian Zock na Birama Ndoye kwa sababu ya club hiyo ilitaka kuwakata mshahara kwa sababu hawachezi Ligi kwa sasa. Naye mshambuliaji wa klabu ya AC Milan ya Italia na aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic juzi alizindua rasmi kampeni ya kufadhili na kusaidia namna ya kupambana na janga la Virusi vya korona. Ibrahimovic ametoa wito kwa wachezaji wenzake kusaidia mapambano dhidi ya kupigana na virusi hivi na kusema ikiwa virusi haviendi kwa Zlatan, Zlatan atakwenda kuvifuata virusi!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako