Mkutano wa kutoa uzoefu wa China juu ya kinga na tiba ya nimonia ya COVID-19 ulifanyika jana na kutangazwa kwa dunia nzima kupitia mtandao wa internet.
Mkutano huo umeshirikisha wataalamu wa China na wa nchi za nje, waliojadili njia za kupambana na virusi vya korona, na kueleza uzoefu wa China kuhusu kinga na tiba ya virusi hivyo. Kwa sasa maambukizi ya virusi nchini China yamedhibitiwa, lakini ugonjwa huo umelipuka na kuenea kwa kasi katika nchi nyingi duniani. Wataalamu wa China wametoa ufumbuzi na hatua mpya za China kuhusu kinga na tiba ya COVID-19.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |