• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Russia wazungumzia kwa simu kuhusu ushirikiano wa mapambano dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-20 09:49:08

    Rais Xi Jinping wa China jana jioni alifanya mazungumzo na mwenzake wa Russia Vladimir Putin kwa njia ya simu.

    Rais Xi amesema kwa sasa hali ya maambukizi ya COVID-19 nchini China inaendelea kuboreshwa, utaratibu wa uzalishaji mali na maisha ya watu umerejeshwa. Amesema China ina imani na uwezo wa kupata ushindi katika vita dhidi ya COVID-19. Pia amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali ikiwemo Russia, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kinga na udhibiti wa virusi hivyo, kubadilishana uzoefu, kuhimiza utafiti wa pamoja wa sayansi, kushirikiana katika kukabiliana na matishio na changamoto za pamoja na kulinda usalama wa afya ya umma katika dunia nzima.

    Rais Putin amesema Russia inapongeza hatua zilizochukuliwa na China na msaada wa China kwa nchi zilizokumbwa na maambukizi ya virusi hivyo, na kuweka mfano wa kuigwa kwa jumuiya ya kimataifa. Pia Russia inapenda kushirikiana na China katika mapambano dhidi ya COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako