• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubalozi wa China wazindua mradi wa kukarabati kituo cha tiba na karantini kwa wagonjwa wa COVID-19 nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2020-03-20 09:50:25

    Ubalozi wa China jana Alhamisi umezindua mradi wa kukarabati upya kituo kikuu cha Zimbabwe cha tina na karantini kwa wagonjwa wa COVID-19 kilichoko mjini Harare, wakati China inaongeza msaada wake kwa nchi hiyo kupambana na virusi vya korona.

    Ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uwezo wa Zimbabwe wa kukabiliana na virusi vya korona, jumuiya ya wafanyabiashara wa China, chini ya mwongozo na uratibu wa Ubalozi wa China, wamehamasisha raslimali kukarabati upya hospitali ya Wilkins mjini Harare ambayo imeteuliwa kuwa kituo kikuu cha tiba ya COVID-19 nchini humo.

    Mpaka sasa Zimbabwe bado haijaripoti maambukizi ya virusi vya korona, lakini imeimarisha maandalizi na mwitikio wake wa kuzuia kuingia kwa virusi hivyo nchini humo.

    Rais Emmerson Mnangagwa Jumanne wiki hii alitangaza mlipuko wa virusi vya korona kuwa janga la taifa, na kupiga marufuku mikusanyiko yote ya watu kwa muda wa siku 60 zijazo ili kuzuia kuenea kwa nimonia ya COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako