• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Wachezaji Ligi Kuu kupimwa corona

    (GMT+08:00) 2020-03-20 16:05:47

    Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), imesema itahakikisha wachezaji wote wanafanyiwa uchunguzi wa maambulizi ya virusi vya corona kabla kushiriki Ligi Kuu Tanzania (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL). Bodi ya Ligi imetoa msimamo huo baada ya watendaji wake kukutana jana kujadili mustakabali wa ligi hizo. Ligi hizo zimesimama kutii agizo lililotolea juzi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye alitangaza uamuzi wa serikali kupiga marufuku kwa siku 20, shughuli zinazosababisha mikusanyiko ikiwemo michezo, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa virusi vya corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako