• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kesi za maambukizi ya COVID-19 barani Afrika zazidi 800

    (GMT+08:00) 2020-03-20 17:42:20

    Kesi za maambukizi ya virusi vya korona COVID-19 barani Afrika zimepita 800 mpaka kufikia leo asubuhi kwa saa za China, na nchi mbalimbali zimeimarisha hatua za kukabiliana na ugonjwa huo unaoenea duniani kwa haraka.

    Kwa mara ya kwanza, Chad, Niger na Cape Verde zimeripoti kesi za maambukizi ya virusi vya Corona. Kati ya nchi za Afrika Mashariki, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nchini Tanzania imeongezeka kwa watu watatu, na nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuongezeka watu wanne.

    Habari zinasema wagonjwa wengi wa COVID-19 barani Afrika wametokea Ulaya, na ili kuzuia ueneaji wa janga hili, nchi mbalimbali barani humo zimesimamisha safari za ndege kutoka nchi zinazokumbwa zaidi na janga hilo haswa nchi za Ulaya.

    Hatua nyingine zisizo kawaida pia zimechukuliwa na nchi za bara hilo. Afrika Kusini imetangaza kuwa, watu wanaoeneza virusi vya Corona kwa makusudi watashtakiwa kwa kosa la mauaji. Tanzania nayo imepiga marufuku kutembelea wafungwa ili kuzuia kuenea kwa virusi gerezani. Serikali ya Zimbabwe imepanga kutenga dola milioni 26.4 za Kimarekani katika kukabiliana na ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako