• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China bara yaripoti hakuna kesi mpya za ndani za maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-20 19:14:34

    Tume ya Taifa ya Afya ya China imesema, hakuna kesi mpya ya maambukizi ya virusi vya Corona zilizoripotiwa China bara siku ya alhamis.

    Tume hiyo imesema, jana ilipokea ripoti ya kesi 39 mpya zilizothibitishwa kuwa na virusi vya Corona, ambazo zote ni za watu waliotoka nje ya nchi. Kati yao, 14 waliripotiwa kutoka mkoa wa Guangdong, nane mjini Shanghai, sita Beijing, na tatu katika mkoa wa Fujian. Miji yenye hadhi ya mikoa ya Tianjin, Liaoning, Heilongjian, Zhejian, Shandong, Guanxi, Sichuan na Gansu kila moja iliripoti kesi moja, na kufanya kesi zilizoingia kutoka nje ya nchi mpaka jana jioni kufikia 228.

    Idadi ya jumla ya kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona China bara ilifikia 80,967 mpaka jana jioni, ikiwemo wagonjwa 6,569 wanaoendelea na matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako