• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yaipongeza China kwa kuiunga mkono katika kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-20 19:14:59

    Serikali ya Ethiopia imeipongeza China kwa kuiunga mkono katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona nchini humo na katika nchi nyingine za Afrika.

    Waziri wa afya wa Ethiopia Lia Tadesse amewapongeza wataalam wa China na Ubalozi wa China nchini Ethiopia kwa kubadilishana nayo uzoefu wa thamani ili kusaidia juhudi zinazoendelea za kuboresha uwezo wa Afrika wa kudhibiti virusi hivyo.

    Ubalozi wa China nchini Ethiopia umesema katika taarifa yake kuwa, China itaendelea kutoa msaada kadri inavyoweza kutokana na mahitaji ya nchi za Afrika. Pia China itaendelea kutekeleza malengo yake katika sekta ya afya chini ya mfumo wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kuboresha uwezo wa Afrika CDC na kuimarisha uwezo wa nchi za Afrika wa kudhibiti na kukabiliana na maambukizi hayo.

    Mpaka sasa kuna kesi sita zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako