• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yajiandaa kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-20 19:15:24

    Serikali ya Uganda imesema nchi hiyo imejiandaa kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na maambukizi ya virusi vya Corona, wakati dunia ikiathirika vibaya kutokana na maambukizi hayo.

    Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Matia Kasaija ameliambia bunge kuwa, nchi hiyo imeathirika na janga la virusi vya Corona, hivyo kuilazimisha kushusha makadirio ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu wa fedha kwa asilimia 0.3 mpaka asilimia 0.8.

    Pia amesema, makadirio hayo yameshushwa kutoka lengo la asilimia 6 kwa mwaka wa fedha 2019/2020, na kuongeza kuwa kama hali itakuwa mbaya zaidi, mamilioni ya Waganda wataingia kwenye umasikini.

    Kasaija amesema, serikali imechukua hatua kukabiliana na athari za virusi vya Corona, pamoja na kuwa hakuna kesi yoyote iliyoripotiwa nchini humo mpaka sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako