• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kauli ya rais wa Marekani ya 'virusi vya China' yaendelea kulaaniwa na jamii ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-03-20 19:28:00

    Kitendo cha rais Donald Trump wa Marekani cha kuita virusi vya korona kuwa virusi vya China kinaendelea kulaaniwa na pande mbalimbali za Marekani na dunia.

    Mjumbe wa masuala ya diplomasia na sera za usalama wa Umoja wa Ulaya, Bw. Josep Borrell Fontelles amesisitiza kuwa, virusi havihusiani na nchi na vinaenea bila kujali mipaka. Virusi vya korona sio virusi vya China, bali ni tishio kubwa kwa jamii ya kimataifa, hivyo ni muhimu watu wote kushirikiana na kuchukua hatua kwa pamoja.

    Mgombea urais wa zamani waMarekani, Bibi Hillary Clinton amesema, maneno ya rais Trump ni ya ubaguzi, na yanalenga kugeuza mawazo ya umma kuhusu kosa lake la kutochukua hatua kwa makini kupambana na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako