• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majimbo manne ya Marekani yatangaza amri ya kukaa ndani

    (GMT+08:00) 2020-03-21 17:57:49

    Majimbo la California, majimbo ya New York, Illinois na Connecticut nchini Marekani yametangaza amri ya watu kukaa ndani. Amri hii inawahusisha mamilioni ya watu kwenye miji mikubwa ya New York, Los Angeles, na Chicago, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.

    Ikulu ya Marekani imetoa taarifa ikisema rais Donald Trump ametangaza kuwa janga kubwa limetokea kwenye jimbo la New York, ikiagiza serikali kutoa misaada kwa jimbo hilo katika kupambana na ugonjwa huo.

    Takwimu mpya kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani zimeonesha kuwa, hadi kufika usiku wa tarehe 20, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona imefikia elfu 20, na 250 wamefariki. Kati ya watu hao, idadi ya wagonjwa wa jimbo la New York inachukua zaidi ya asilimia 40.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako