• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haijawa na maambukizi mapya ya ndani ya virusi vya Corona kwa siku tatu mfululizo

    (GMT+08:00) 2020-03-21 18:02:20

    Mamlaka ya afya ya China imesema kwa siku ya tatu mfululizo sasa China bara imekuwa na maambukizi mapya sifuri ya ndani.

    Kamisheni ya afya ya taifa imesema jana Ijumaa ilikuwa imepokea ripoti za maambukizi 41 mapya kutoka nje ya nchi,14 mjini Beijing, 9 mjini Shanghai, 7 katika mkoa wa Guangdong, manne mkoa wa Fujian, Shangdong na Shaanxi mawili kila mmoja, na mkoa wa Sichuan mtu mmoja. Hadi kufikia jana jumla ya maambukizi mapya kutoka nje yamefikia 269.

    Wakati dunia ikiendelea kupambana na virusi vya Corona mkurugenzi wa shirika la afya duniani (WHO) Bw. Tedros Ghebreyesus amezitaka nchi zote duniani kuiga moyo wa China kwenye mapambano dhidi ya virusi hivyo ulioonyeshwa mjini Wuhan. Amesema mafanikio yaliyopatikana katika mji huo yanaonyesha kuwa dunia inaweza kushinda vita dhidi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako