• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washauri wa kisiasa washauri kupigwa marufuku ulaji wa wanyamapori

    (GMT+08:00) 2020-03-21 18:02:43

    Wajumbe wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China jana walikutana kwenye semina kushauri kupigwa marufuku desturi ya baadhi ya watu kula wanyama pori.

    Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya Baraza la mashauriano ya kisiasa la China (CPPCC) Bw. Wang Yang aliyekuwa mwenyekiti wa semina hiyo, alitoa hotuba na kusema elimu na faini vyote vinatakiwa kuongezwa ili kuongeza mwamko wa umma kuacha kula wanyama pori.

    Bw. Wang amewataka wajumbe hao wenyewe kuwa mfano na kuepuka matumizi ya nyama hiyo, na kuchangia busara zao na nguvu zao kuondoa tabia hiyo kwenye jamii. Wajumbe pia wamependekeza kuwa maudhui kuhusu kulinda wanyama pori na kulinda afya ya umma, vinatakiwa kuwepo kwenye mitaala ya elimu ya lazima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako