• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Australia aona idadi kubwa ya wagonjwa wa Corona nchini humo inahusiana na Marekani

    (GMT+08:00) 2020-03-22 18:20:53

    Waziri mkuu wa Australia Bw. Scott Morrison hivi karibuni alipofanyiwa mahojiano na kituo cha redio ya nchi hiyo amesema sababu kuu ya ongezeko la idadi ya wagonjwa wa Corona nchini humo ni kutodhibitiwa kwa idadi ya wagonjwa wanaotoka nje ya nchi, akisema:

    "Nchi moja inatakiwa kuwajibika na Australia. Idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya Corona wanatoka nje ya Australia au kuwasiliana na watu waliorudi kutoka nchi za kigeni, na wengi wao wanatoka Marekani. "

    Msomi maarufu wa Australia Bw. Colin Patrick Mackerras anasema China imekuwa ikifanya juhudi kubwa kadiri iwezavyo katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, hakuna sababu yoyote ya kuilaumu, akisema:

    "Nimesikia mashaka ya Marekani dhidi ya China, haswa msimamo wa rais Donald Trump ni mkali, lakini China haikuathiriwa nao na kushinda shida kubwa. Naamini kuwa China itafanya vizuri zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako