• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa Italia asema virusi vinavyofanana sana na COVID-19 vilianza kutokea mwishoni mwa mwaka jana nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-03-22 18:21:49

    Hivi karibuni mtaalamu mashuhuri wa matibabu wa Italia Bw. Giuseppe Remuzzi alipofanyiwa mahojiano na Redio ya Taifa ya Marekani NPR amesema, kuna uwezekano kuwa nimonia inayofanana sana na ile inayosababishwa na virusi vya Corona COVID-19 ilianza kutokea mwezi Novemba na Disemba mwaka jana nchini humo.

    Amesema alipata habari mpya kutoka kwa madaktari kuwa walikuwa wamekutana na nimonia ya ajabu tena mbaya sana kutoka kwa wazee mwezi Novemba na Disemba mwaka jana, hali ambayo inaonesha kuwa kabla ya maambukizi ya virusi vya Corona kulipuka nchini China, virusi hivyo vilikuwa vimeenea kwenye eneo la Lombardia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako