• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yawasihi wananchi kuwa watulivu baada ya mgonjwa wa kwanza wa virusi vya Corona kuthibitishwa

    (GMT+08:00) 2020-03-22 18:22:28

    Wizara ya Afya ya Uganda leo imewataka wananchi wawe watulivu baada ya nchi hiyo kuthibitisha mgonjwa wa kwanza wa virusi vya Corona.

    Kwenye taarifa yake, Wizara ya Afya ya nchi hiyo imesema mgonjwa huyo ambaye ni Mganda mwanamume mwenye miaka 36, ametambuliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe, na baadaye kutengwa. Mtu huyo alipimwa na kuonekana na virusi vya Corona baada ya kuwasili Uganda akitokea Dubai Jumamosi, ambaye alipanda ndege ya Ethiopia akiwa na dalili za homa kali na kupoteza hamu ya kula. Wizara hiyo pia imesema orodha ya abiria imepatikana na wahusika wote wametafutwa, na kwamba wanashikilia pasipoti za abiria wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

    Jana Jumamosi rais wa Uganda Yoweri Museveni alitangaza kufungwa kwa mipaka yote ili kuzuia virusi hivyo vya Corona kusambaa nchini. Na hakuna abiria atakayeruhusiwa kuingia Uganda si kwa njia ya anga, maji au ardhini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako