• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa afya wa China waeleza uzoefu wao kwa wenzao wa nje katika kutibu virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-22 18:22:52

    Wataalamu wa China wa dawa za mitishamba na za magharibi wameeleza uzoefu wao kwa njia ya video na wenzao wa Italia, Marekani, Ubelgiji, Japan na Shirika la Afya Duniani katika kutibu wagonjwa wenye virusi vya Corona.

    Daktari wa magonjwa ya moyo wa Hospitali ya Tongji ya Wuhan ambako ndio kitovu cha mlipuko, amesema uzoefu mkubwa wa China ni kuwalaza wagonjwa wote hospitali. Amefafanua kuwa kwa vile virusi vya Corona vinasambaa kwa kasi, kumuweka karantini nyumbani mgonjwa mwenye dalili za wastani ni sawa na kusambaza moto kila mahali, ambapo hatimaye utapelekea maambukizi ya familia nzima. Ushauri huo umeungwa mkono na mkurugenzi wa kitengo cha magonjwa ya mfumo wa hewa cha Hospitali ya Guang'anmen ya Beijing Li Guangxi, ambaye anaamini kwamba wagonjwa wanapaswa kupata matibabu mapema. Amesema wanapaswa kutilia mkazo wiki ya kwanza ya ugonjwa kwani hiyo ni nafasi nzuri ya kuzuia ugonjwa usikue kutoka wastani hadi kuwa mkali zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako