• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yaimarisha hatua za kupambana na virusi vya Corona wakati idadi ya wagonjwa ikizidi elfu moja

    (GMT+08:00) 2020-03-22 18:26:46

    Nchi mbalimbali za Afrika zimeongeza hatua za kupambana na virusi vya Corona ikiwemo kufunga mipaka, kutengwa kwa lazima, na kupiga marufuku mikusanyiko ya umma, wakati maambukizi yaliyothibitishwa ya virusi yakifikia zaidi ya 1,100 katika nchi na sehemu zaidi ya 40 barani humo baada ya Angola, Eritrea na Uganda kutangaza kesi za kwanza.

    Cote d'Ivoire, Sao Tome and Principe, Togo, Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo DRC, Uganda na Gambia zimetangaza kufunga mipaka ya nchi na kusimamisha safari zote za ndege za kimataifa kwa muda tofauti.

    Tanzania na Zambia zimeongeza hatua za kupambana na habari feki zinazohusiana na maambukizi ya virusi vya Corona, na wanaosambaza uvumi kwenye mitandao ya kijamii watachukuliwa hatua za kisheria.

    Serikali ya Kenya itatenga Shilingi za Kenya bilioni moja, sawa na dola za kimarekani milioni 9.4 kuwaajiri wafanyakazi wa matibabu na afya na serikali ya Guinea Ikweta itatoa CFA franc bilioni 5, sawa na dola za kimarekani milioni 8.1 kama mfuko wa dharura wa kupambana na virusi vya Corona.

    Cameroon na Angola zimewataka watu walio karibu na wagonjwa waliothibitika kuwa na virusi vya Corona wakubali kupimwa au kujitenga nyumbani, la sivyo huenda watakiuka sheria.

    Burkina Faso, Malawi, Togo, Rwanda nazo zimetangaza kupiga marufuku mikusanyiko ya watu kwa viwango tofauti, kufunga shule au hifadhi za taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako