• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema uchumi wa China unarudi tena kwenye hali ya kawaida

    (GMT+08:00) 2020-03-22 18:27:27

    Shirika la Fedha Duniani IMF tarehe 20 lilitoa waraka uitwao "Uzoefu wa China katika kupunguza athari mbaya inayosababishwa na Corona", ambao unaona kuwa sera mwafaka inaweza kufanya kazi muhimu katika kupambana na Corona na kupunguza athari mbaya inayotokana na virusi hivyo, China imeanza tena kazi kama kawaida, uchumi wa nchi unaanza kurudi tena kwenye hali ya kawaida, hali ambayo inaweza kupunguza ugumu wa uchumi wa dunia.

    Waraka huo unasema kuenea kwa Corona kumeleta athari mbaya kwa uchumi wa dunia, China imechukua hatua mwafaka haraka iwezekanavyo na kusaidia kupunguza athari hiyo.

    Mwandishi wa waraka huo ambaye ni mkurugenzi wa IMF anayeshughulikia mambo ya China Bw. Helge Berger amesema, kama mkurugenzi mkuu wa IMF Bibi Kristalina Georgieva alivyosema uchumi wa China una nguvu, ambao unaweza kurudi tena kwenye hali ya kawaida chini ya sera mwafaka ya serikali ya China. Berger pia ametoa wito kwa nchi zote duniani zishirikiane kwa ngazi mbalimbali, ili kupambana na Corona kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako