• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wengi wa Marekani wauza hisa kabla ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-22 21:29:08

    Vyombo vya habari vya Marekani hivi karibuni vimeripoti kuwa, wabunge wengi wa majimbo mbalimbali nchini humo yakiwemo North Carolina, California, Oklahoma na Georgia, waliuza hisa zao kabla ya soko la hisa kuporomoka kwa kiasi kikubwa hivi karibuni.

    Kwa mujibu wa Redio ya Taifa ya Marekani NPR, mbunge wa Jimbo la North Carolina Bw. Richard Burr ni mmoja kati ya watu hao. Bw. Burr ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya upelelezi ya baraza la juu la bunge, na mwanachama wa Kamati ya afya ya baraza hilo, anasikiliza taarifa kuhusu hali ya maambukizi ya virusi vya Corona kila baada ya muda.

    Rekodi ya hisa imeonesha kuwa, Bw. Burr na mke wake waliuza hisa 33 zenye thamani ya dola za kimarekani kati ya laki 6.28 na milioni 1.7 tarehe 13 Februari, kitendo chake hicho kiliripotiwa hadi kufikia tarehe 27 Februari.

    Rekodi ya siri iliyotolewa na NPR imeonesha kuwa, tarehe 27 Februari Bw. Burr alionya wakazi wa jimbo lake la uchaguzi wenye uhusiano mzuri naye kuwa, maambukizi ya virusi vya Corona yanaenea kwa kasi zaidi kuliko virusi vingine vyote katika historia. Lakini siku hiyo rais Trump alijaribu kuwatuliza watu kwamba virusi hivyo vitatoweka kama muujiza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako