• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aliyekuwa afisa mwandamizi wa Marekani amkosoa Trump kwa kuvunja ofisi inayoshughulikia magonjwa ya kuambukiza

    (GMT+08:00) 2020-03-22 21:38:33

    Gazeti la The Independent la Uingereza limesema aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Susan Rice amemkosoa rais Donald Trump wa Marekani kwa kutojiandaa vya kutosha kupambana na virusi vya Corona vinavyoenea dunia nzima, licha ya tahadhari nyingi kutolewa kabla..

    Rice amesema hayo alipohojiwa na Shirika la Utangazaji CNN kwa njia ya simu. Rice alionesha umuhimu mkubwa katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Ebola alipoihudumia serikali ya Marekani iliyoongozwa na Barack Obama. Katika kipindi cha mpito, timu ya Rice iliwahi kutoa tarifa kwa ofisa ya serikali ya Trump juu ya uwezekano wa kutokea tena kwa magonjwa ya kuambukiza. Ikiwa sehemu ya kazi hiyo, timu yake ilifanya mazoezi na kujadili jinsi ya kukabiliana na kutokea kwa magonjwa yanayoishambulia dunia nzima.

    "tunajua hii ni hatari kubwa na inayoweza kutokea" " hii ndio sababu tulianzisha ofisi inayoshughulikia usalama wa afya na ulinzi wa kibailojia duniani chini ya uongozi wa Obama. Tuliteua ofisa mwandamizi aliyepewa madaraka ya kutoa ripoti moja kwa moja kwa mshauri wa usalama wa taifa na mshauri wa usalama wa ardhi. Lakini ofisi hiyo ilivunjwa miaka miwili iliyopita." alisema Bi. Rice kwenye mahojiano hayo.

    Hatua ya serikali ya Trump kuvunja ofisi hiyo mwaka 2018 ilidhaniwa kuwa ni moja ya sababu zinazokwamisha juhudi za serikali za kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona nchini humo.

    Aidha, habari zinasema rais Trump alitetea kuchelewa kwa serikali yake kupambana na virusi vya Corona akisema virusi hivyo vimekuja ghalfa kiasi cha dunia kushindwa kuitikia. "kauli hii sio sahihi. sio tu tunajua vitalipuka, pia tunatakiwa kujiandaa vya kutosha kama ilivyofanya serikali ya Trump, na pia serikali ya Trump ina fedha za kutosha kukabiliana navyo." alikanusha Bi.Rice

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako