• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Angela Merkel ajiweka kwenye karantini baada ya daktari aliyemuona kuthibitika kuwa na virusi vya corona

    (GMT+08:00) 2020-03-23 09:04:19

    Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel amejiweka kwenye karantini nyumbani na atafanyiwa vipimo vya virusi vya corona katika siku kadhaa zijazo, baada ya daktari mmoja aliyemuona kuthibitika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

    Msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffen Serbert amesema Bibi Merkel aliarifiwa baada ya mkutano na wanahabari kwamba daktari aliyempa chanjo ya nimonia alithibitika kuwa na maambukizi yonayosababishwa na virusi vya corona.

    Kabla ya hapo Bibi Merkel alitangaza kupiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya wawili, ikiwa ni sehemu ya hatua za kudhibiti mlipuko wa virusi vya Corona nchini Ujerumani. Hadi kufikia jana Ujerumani imeripoti vifo 90 na maambukizi zaidi ya 24,100 ya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako