• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mask na vifaa vya upimaji vilivyotolewa na Mfuko wa Jack Ma vyawasili Ethiopia

    (GMT+08:00) 2020-03-23 09:35:41

    Vifaa vingi vya matibabu vilivyotolewa na Mfuko wa Jack Ma kwa nchi 54 za Afrika, vimewasili Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia kupitia ndege ya mizigo ya Shirika la ndege la Ethiopia.

    Vifaa hivyo ni pamoja na mask milioni 5.4, vitendanishi milioni 1.08, seti 40,000 za nguo za kujikinga na seti 60,000 za miwani ya kujikinga. Kwa mujibu wa Mfuko wa Jack Ma, Vifaa hivyo vitasambazwa kwanza kwa nchi za Afrika ambazo zina hatari zaidi ya maambukizi ya virusi vya Corona. Na mask 600,000 zaidi zinatarajiwa kufika Addis Ababa na kusambazwa kwa nchi zaidi barani Afrika katika wiki chache zijazo.

    Waziri wa afya wa Ethiopia Lia Tadesse ameshukuru msaada wa Mfuko wa Jack Ma, vilevile amesema Ethiopia imekuwa inapokea vifaa vya matibabu na pia kuiga uzoefu wa China.

    Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika. Balozi wa Afrika Kusini nchini Ethiopia Bw. Edward Makaya amesema, mchango huo sio kama tu utasaidia Afrika Kusini, bali pia bara lote, kujenga uwezo wa kupambana na virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako