• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Beijing Raiders kuiwakilisha Nairobi kwenye fainali za Chapa Dimba na Safaricom Season Three

    (GMT+08:00) 2020-03-23 09:43:00

    Kwa mara ya pili timu ya wasichana ya Beijing Raiders itawakilisha Mkoa wa Nairobi kwenye fainali za kitaifa za Mashindano ya Chapa Dimba na Safaricom Season Three mwaka huu. Kikosi hicho kitashiriki fainali za kitaifa kwa mara ya pili baada ya kushiriki fainali za kipute hicho cha Season One mjini Kakamega. Beijing Raiders ilitwaa tiketi ya kushiriki kinyang'anyiro cha mwaka huu ilipoibuka malkia wa Mkoa wa Nairobi. Kina dada hao wa kocha, Mark Okwiri waliibuka malkia baada ya kuteremsha soka ya kuvutia na kuchoma wapinzani wao bila huruma kwenye fainali zilizoandaliwa katika Shule ya Upili ya Jamhuri High, jijini Nairobi. Fainali za kipute hicho zimepangwa kuandaliwa mjini Mombasa mwezi Juni mwaka huu ingawa huenda mlipuko wa virusi vya corona ukachangia kusukumwa mbele. Mabingwa katika fainali za kitaifa wavulana na wasichana kila moja atatuzwa kitita cha Sh1 milioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako