• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OLIMPIKI: IOC yajipa wiki nne tu kuamua kuhusu michezo ya Olimpiki ya Tokyo kufuatia virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-23 09:43:16

    Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC inafikiria kuahirisha michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020, na imejipa hadi wiki nne tu kutoa maamuzi hayo. Bodi tendaji ilikutana jana kufuatia kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa kamati za nchi mbalimbali za wanariadha na olimpiki, kutaka michezo hiyo icheleweshwe kwasababu ya mlipuko wa virusi vya corona. Kamati hiyo imesema suala la kufuta kabisa michezo hiyo halipo kwenye ajenda yake bali watajadili kama wafuate mpango wa sasa wa kuanza michezo hiyo Julai, 24 2020 au kubadilisha na kuanza baadaye. Hata hivyo kuahirishwa kwa miezi kadha au pengine kwa mwaka mzima inafikiriwa kuwa ndio njia nzuri. Wadau wa Olimpiki wanataka uamuzi huo utolewe haraka ili kuondoa sintofahamu kwa wanariadha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako