• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Teknolojia ya China yasaidia Kenya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-23 09:45:21

    Kituo cha teknolojia ya matibabu kutoka mbali cha Kenya kimezinduliwa katika Hospitali ya Kenyatta mjini Nairobi. Kituo hicho kinachotumia teknolojia ya China kitazisaidia nchi za Afrika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

    Kwenye hafla ya uzinduzi, madaktari wa Kenya waliwasiliana na madaktari walioko katika miji ya Beijing na Wuhan kwa kutumia teknolojia hiyo, kubadilishana uzoefu katika kupambana na ugonjwa huo.

    Waziri wa Afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe amesema mawasiliano hayo yaliyofanyika kwa kutumia teknolojia ya mbali yana umuhimu mkubwa kwa Kenya, na kwamba kubadilishana uzoefu na madaktari wa China, kunaweza kuisaidia Kenya kuzuia na kudhibiti ugonjwa, na kupunguza athari mbaya za ugonjwa huo kwa Kenya. Amesema anatarajia kuimarishwa kwa mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya matibabu, ili kuwanufaisha wakenya na binadamu wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako