• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya China yaichangia Rwanda vifaa na fedha kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-23 09:56:14

    Makampuni ya China yameichangia serikali ya Rwanda vifaa na fedha ili kuiunga mkono Rwanda katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Kampuni ya ujenzi China Star imeipatia wizara ya afya ya Rwanda vitendanishi vya upimaji vinavyoweza kuwahudumia watu takriban 100. Mkuu wa kampuni hiyo anayeshughulikia mambo ya Afrika Mashariki Bw. Chen Lisheng amesema kampuni yake inaandaa kuipatia Rwanda vifaa vingine, ikiwa ni pamoja na mask, nguo za kujikinga na vitendanishi.

    Shirikisho la mapampuni ya China nchini Rwanda limeichangia wizara ya afya ya Rwanda dola elfu 11 za kimarekani. Mkurugenzi wa shirikisho hilo Bw. Li Jianbo amesema makampuni ya China yanapaswa kushirikiana na Rwanda katika kupambana na virusi kwa pamoja.

    Mbali na hayo, kampuni ya teknolojia ya matibabu ya China Tiankang jana iliupatia ubalozi wa China nchini Rwanda mask na nguo za kujikinga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako