Klabu ya Real Madrid imeamua kutomsajili kiungo wa Machester United, Paul Pogba. Hatua hiyo imefikiwa baada ya timu ya Man United kutaka pesa ndefu ili kumuuza mchezaji huyo, huku Real Madrid ikiamini kuwa thamani ya mchezaji huyo kwa sasa imeshuka. Man United inataka kumuuza mchezaji huyo kwa Euro milioni 200, lakini Real Madrid wanaona kiungo huyo hastahili kuuzwa kwa bei kubwa kama hiyo. Sababu nyingine ya kumuacha kiungo huyo ni majeraha ya mara kwa mara aliyopata Pogba yaliyomfanya kuwa nje kwa muda mrefu katika msimu huu, hivyo kuhisi kuwa huenda kiwango chake katika soka kimeshuka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |