• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Simba Yamkomalia Mzambia wa Orlando Pirates

    (GMT+08:00) 2020-03-23 16:09:29

    Uongozi wa Simba umependekeza majina mawili ya wachezaji wa kuwasajili, akiwemo Benard Morrison wa Yanga au Justin Shonga wa Orlando Pirates. Baada ya kumkosa Morrison ambaye amesaini mkataba wa kuendelea kuichezea Yanga kwa miaka miwili zaidi, sasa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara wamemkomalia Shonga mwenye uraia wa Zambia. Simba chini ya Kocha Sven Vandenbroeck, wanafahamu kuwa watashiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, hivyo wanahitaji mchezaji ambaye ataongeza nguvu katika kikosi chao haswa katika eneo la ushambuliaji ambapo kwa sasa eneo hilo linachezwa na washambuliaji wawili pekee, Meddie Kagere na John Bocco.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako