• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema sera ya kifedha ya China ni funzo muhimu kwa nchi zilizoathiriwa zaidi na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-23 17:39:51

    Mkuu wa ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nchini China Helge Berger amesema, moja ya mafunzo muhimu kutoka kwa uzoefu wa China ni kwamba ni muhimu kuwa na sera za kiuchumi zitakazolenga kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na virusi vya corona (COVID-19) na kusaidia ufufukaji.

    Amesema China inafanya juhudi kubwa za kifedha zinazolenga kusaidia familia zilizo hatarini na kampuni ndogo zilizoathirika zaidi na mlipuko huo huku sera za kifedha zikidumu kuwa chanya. Pia amesema, Benki Kuu ya China imetoa fedha za kutosha katika masoko ya fedha na katika mabenki, kushusha riba, na kujitahidi kupeleka fedha kwenye kampuni zilizo chini ya shinikizo ili kuhamasisha uzalishaji wa vifaa vya tiba.

    Akizungumzia athari za mlipuko wa virusi vya corona kwa uchumi wa China, Berger amesema athari ya ghafla ya mlipuko huo ni kusimamishwa kwa uzalishaji katika robo ya kwanza ya mwaka, lakini habari njema ni kwamba, uchumi wa China uko katika mwelekeo wa kurejea hali yake ya kawaida, na kwamba ufufukaji dhahiri utaonekana katika robo ya pili ya mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako