• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaahidi kuendelea kusaidia nchi za Afrika kupambana na virusi vya corona

    (GMT+08:00) 2020-03-23 21:12:24
    China imeahidi kuongeza nguvu ya kusaidia nchi za Afrika kupambana na virusi vya corona, ikiwa ni ishara ya kuzishukuru nchi za bara hilo kwa kuiunga mkono China katika kukabiliana na virusi hivyo, na kutafsiri kwa vitendo uhusiano wa kirafiki, kiwenzi na kindugu kati ya pande hizo mbili.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang leo hapa Beijing amesema China inafuatilia kwa karibu maambukizi ya virusi vya corona barani Afrika. Pia China imejitahidi kutoa misaada ya vitu kwa nchi za Afrika na Umoja wa Afrika ikiwemo vifaa vya kupima virusi na vifaa vya kujikinga, kuwahimiza wataalam wake kufanya mkutano kwa njia ya video na wenzao wa Afrika, na kuvihamasisha vikosi vya msaada wa matibabu vya China barani Afrika kushiriki kwenye juhudi za nchi mbalimbali za kupambana na virusi hivyo.

    Geng ameongeza kuwa, misaada hiyo ya dharura inayotolewa na serikali ya China itawasili Afrika kwa awamu, na China itaendelea kuratibu na kuhimiza makampuni yake na asasi za kiraia kutoa misaada husika kwa nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako