• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la Ndege la Kenya lasitisha safari zote za kimataifa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-23 21:15:09

    Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) limesema leo kuwa limesitisha safari zote za ndege za kimataifa kuanzia jumatano usiku mpaka itakapotangazwa tena, ikiwa ni juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Allan Kilavuka amesema, safari za ndege za mizigo zitaendelea kutoa huduma za dharura na kusafirisha mahitaji, na kwamba safari za ndege kati ya Mombasa na Kisumu zitaendelea.

    Wakati huohuo, Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe amesema, wageni wote wanaoingia nchini humo kati ya jumapili mpaka jumatano watawekwa kwenye karantini katika sehemu iliyotengwa na serikali na wanatakiwa kujilipia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako